Malengo ya Kozi ya EKP
Lengo kuu la kozi ya EKP ni kuwawezesha watu kuujua Uislamu kwa usahihi wake na kuwa tayari
kuishi kiislamu katika kukiendea kila kipengele cha maisha yao ya kila siku ya kibinafsi na kijamii.
Pamoja na lengo hili kuu, malengo makhsusi ya kozi ya EKP ni :
Kuwaandaa waislamu kulingania na kuhuisha Uislamu katika jamii.
Kuwawezesha wanafunzi wa kidato cha nne na wale wa Cheti na Diploma ya Ualimu kujiandaa vyema kwa mitihani ya taifa ya Elimu ya Dini ya Kiislamu (EDK) .
Kuwaandaa na kuwawezesha waalimu waislamu katika shule za msingi na sekondari kufundisha somo la EDK katika shule zao.
Mpangilio wa Kozi ya EKP ‘online’
Kozi ya EKP ‘online’ itatolewa kutokana na juzuu saba (7) za EKP ambazo masomo yake yamegawanywa katika fani nne zifuatazo.
Tawhiid
Fiqh
Tarekh
Da’awah
Mahusiano ya hizi fani nne na juzuu saba (7) za EKP zimeainishwa katika jedwali lifuatalo:
NA
FANI
JUZUU
GHARAMA
1
Tawhiid
1
@ 2000/=
2
Fiqh
2,3 na 4
@ 2000/=
3
Tarekh
5 na 6
@ 2000/=
4
Da’awah
7
@ 2000/=
Kozi itaendeshwa kwa kufuata mtiririko wa juzuu kuanzia ya kwanza hadi ya saba. Kila juzuu
itagawanywa katika masomo yenye mada mbalimbali